KAMPALA:Mazungumzo ya amani nchini Uganda kuendelea
23 Februari 2005Matangazo
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na waasi wa LRA yataendelea wiki ijayo hata baada ya kumalizika kwa muda wa msamaha.
Msaha huo uliotolewa na rais Yoweri Museveni ulimalizika jumanne na oparesheni za kijeshi zinatarajiwa kuanza upya.
Lakini serikali ya Uganda imesisitiza kwamba juhudi za kumaliza uhasama uliosababisha vita vya miaka 18 kaskazini mwa Uganda zitaendelea.