KAMPALA:Mazungumzo baina ya serikali ya Uganda na waasi yameahirishwa hadi kesho
13 Agosti 2006Matangazo
Mazungumzo ya kuleta amani baina ya waasi na serikali ya Uganda yanatarjiwa kuanza tena hapo kesho nchini Sudan baada kuahirishwa kutokana na pande mbili hizo kushindwa kukubaliana juu ya kusimamisha mapigano.
Waasi hao wa LRA walitangaza hatua ya kusimamisha mapigano hapo awali lakini walikataa kuhudhuria mazungumzo zaidi ili kuitaka serikali ya Uganda nayo isimamishe mapigano.
Pande mbili hizo bado hajizakubuliana kwa uhakiha juu ya utaratibu wa kusimamisha vita.