KAMPALA:Kiongozi wa upinzani akamatwa Uganda
15 Novemba 2005Matangazo
Maafisa nchini Uganda wamemkamata mtu alietazamiwa kutoa changamoto kali kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda katika uchaguzi wa kwanza kuruhusu zaidi ya chama kimoja cha kisiasa tangu miaka 20.Kiongozi wa upinzani,Kizza Besigye ameshtakiwa makosa ya uhaini baada ya kukamatwa.Siku ya Juamatatu,polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa Besigye walioandamana barabarani kwa mamia.Ripoti isiyothibitishwa inasema kulitokea kifo kimoja.Wiki chache za nyuma Besigye alipokewa kwa shangwe kubwa aliporejea nyumbani kutoka Afrika ya Kusini ambako alikuwa uhamishoni kwa miaka 4.Hapo zamani Besigye alikuwa daktari wa Museveni na rafiki wake mkubwa.