KAMPALA:Human Rights Watch lailaumu serikali ya Uganda kwa kuwatia ndani wabunge wawili wa upinzani
28 Aprili 2005Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini Neyork Marekani la Human Rights Watch, limesema kukamatwa na kuwekwa ndani kwa wabunge wawili wa upinzani nchini Uganda kwa madai ya kuhusika katika mauji, kumesababisha kutulia kwa wingu la kisiasa katika uchaguzi ujao wa kwanza wa vyama vingi baada ya kipindi cha miaka 20 ya kuwa na chama kimoja.
Ronald Reagan Okumu na Michael Nyeko Ocula walikamatwa wiki iliyopita kwa madai ya kumua meneja wa kampeini ya rais Museveni miaka mitatu iliyopita katika wilaya ya Gulu,Uganda ya Kaskazini.Wabunge hao wamekanusha mashtaka huku wafuasi wao wakisema kuzuiliwa kwao ni mpango wa serikali ya Uganda ili kuutatiza upinzani katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Marchi mwakani.
Kwa mujibu wa mtafiti wa masuala ya Afrika katika shirika hilo la Human Rights Watch Jamera Rone,kuwekwa ndani kwa wabunge hao bila ya kushtakiwa huenda kukawazuia kufanya kampeini zao kabla ya uchaguzi.
Kesi dhidi ya wawili hao ilihairishwa hadi May 6 baada ya wasimamizi wa mashtaka kutaka muda zaidi wa kufanya uchunguzi.Lakini hata hivyo serikali ya Uganda imekanusha kukamatwa kwa wabunge hao wa chama cha upinzani cha Forum For Demokratic Change kumechochewa kisiasa.