KAMPALA.Bunge lapitisha mswada wa rais wa Uganda kukaa mamlakani bila kipimo
29 Juni 2005Matangazo
Bunge nchini Uganda limepiga kura ya kuidhinisha rais wa nchi hiyo kutawala bila muhula maalum, hatua ambayo sasa itamuwezesha rais Yoweri Kaguta Museveni kuendelea kutawala.
Spika wa bunge la Uganda bwana Edward Ssekandi aliwaambia wabunge waliopinga wasikate tamaa kwani mswada huo utawasilishwa tena bungeni baada ya mwezi mmoja.
Wabunge 232 waliunga mkono mswada huo dhidi ya wabunge 50 ambao waliupinga.
Mamia ya ya watu walifanya maandamano nje ya Bunge kupinga mswada huo.
Rais Museveni hajatamka iwapo ana nia ya kutaka kuendelea kuwepo madarakani.