Kampala: Wanavijiji wasema watu 53 wameuliwa na waasi Waasi ...
19 Novemba 2003Matangazo
wamewaua watu 17 kwa uchache kaskazini mwa Uganda, afisa wa ngazi ya juu wa serikali alisema hiyo jana, huku wakazi wakiripoti vifo vya wanavijiji 53 katika wilaya hiyo hiyo. Egou Engwau, kamisha wa wilaya ya Lira, alisema waasi walishambulia Ngetta na Okodi jumatatu na jumanne. Aliliambia shirika la habari la Reuters, kwamba amewatuma maafisa wa usalama kuthibitisha ripoti za mauaji mengine katika mji wa Lira, kadiri ya maili 190 kaskazini mwa mji mkuu Kampala. Hapo awali, kasisi ya kikatoliki anayeishi Lira, alisema wakaazi waligundua maiti 53 baada ya waasi kushambulia vijiji katika wilaya ya Lira.