KAMPALA. Wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere waleta vurumai
11 Novemba 2005Wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda leo wamefanya fujo kupinga ongezeko la malipo ya mitihani.
Wanafunzi hao walichoma magari, kupora maduka na kufanya ghasia zingine.
Kituo kimoja cha kibinafsi cha radio kimeripoti kuuwawa kwa wanafunzi wawili lakini naibu wa msemaji wa polisi nchini Uganda bwana Patrick Onyango amekanusha kuuwawa kwa mwanafunzi yoyote katika ghasia hizo.
Bwana Onyango pia ameeleza kwamba wanafunzi kadhaa wamejeruhiwa kataika patashika hiyo polisi wa kupambana na ghasia walipofyatua risasi za plastiki na mabomu ya kutoa machozi kwa ajili ya kuwatawanya wanafunzi hao.
Wanafunzi wanapinga ongezeko la malipo ya kurudia mitihani kutoka shilingi alfu 60 hadi shilingi alfu mia moja na ishirini za Uganda, sawa na dola 66 za kimarekani.