KAMPALA :Wanachi wa Uganda wapiga kura ya maoni leo
28 Julai 2005Matangazo
Vyama vya siasa na jumuiya za upinzani zimetoa mwito wa kususia kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika leo nchini Uganda juu ya kurejesha mfumo wa vyama vingi vya siasa baada ya jumuiya hizo kushindwa kuzuia kura hiyo kwa njia za kisheria.
Vyama na jumuiya hizo zimesema kura hiyo ya maoni ni ya gharama kubwa na kwamba inafanyika kinyume cha sheria.
Iwapo wananchi watasema ndio , mfumo wa vyama vingi vya siasa utarejeshwa nchini Uganda baada ya kupigwa marufuku kwa muda wa miaka 19 iliyopita.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwaka kesho.
Hatahivyo wahakiki wamesema kwamba zoezi la leo ni njama zenye lengo la kudumisha utawala wa rais Yoweri Museni.
.