Kampala. Uganda yasitisha leseni ya utangazaji kwa kituo kimoja cha radio ya FM.
12 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Uganda imesitisha leseni ya kufanya shughuli za utangazaji kwa radio moja ya FM nchini humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya radio hiyo maarufu kutangaza kipindi kilichojadili nadharia juu ya kifo cha makamu wa rais wa Sudan John Garang.
Kiongozi huyo wa zamani wa waasi aliuwawa wakati helikopta ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ilipoanguka hapo Julai 30.
Mapema hapo jana Alhamis mjini Khartoum , Salva Kiir aliapishwa kuwa makamu wa rais wa Sudan , akichukua mahali pa John Garang.
John Garang ameongoza majeshi ya kusini mwa Sudan katika vita vya miongo miwili ambapo zaidi ya watu milioni mbili waliuwawa.