KAMPALA: Uganda yaomba ruhusa iwapeleke wanajeshi wake nchini Kongo Kinshasa
20 Oktoba 2005Matangazo
Uganda imeomba idhini rasmi kutoka kwa majirani zake iruhusiwe kuwapeleka wanajeshi wake mashariki wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kuwasaka waasi wa kundi la Lords Resistance Army, LRA, wanaotafuta ufadhili kwenye eneo hilo.
Siku moja baada ya umoja wa mataifa kutangaza kwamba serikali ya Kinshasa na serikali ya Kampala zingeunda kikosi cha pamoja kutathmini ni wapi wanakojificha waasi hao, waziri wa mambo ya kigeni wa Uganda, Sam Kuteesa amependekeza kupanuliwa kwa operesheni hiyo.
Ameuambia mkutano kuhusu usalama katika eneo la maziwa makuu, kwamba waasi wa LRA wamekuwa wakifanya harakati zao nje ya Sudan kwa miaka 10 na sasa wanataka kuingia mashariki mwa Kongo Kinshasa.