Kampala: Ndugu wa rais wa Uganda akabiliwa na mashataka
13 Novemba 2003Matangazo
Baraza la mawaziri nchini Uganda limetoa wito wa kushtankiwa nduguye rais, kwa kujumuika katika hasara ya Dolla milioni saba kwenye mkataba wa serikali wa kununua helikopta za kijeshi, alisema afisa wa ngazi ya juu hii leo. Baraza la mawaziri linachukua hatua hiyo kufuatia mapendekezo yaliyotolewa mwaka jana na tume ya uchunguzi ya kisheria mwaka 1997 kuhusu mkataba huo, ambamo jeshi lilimtumia mchuuzi anunue helikopta mbili kutoka Belarus mbazo hazikufaa kusafiri. Mkataba huo ulitayarishwa mnamo wakati ambao Uganda ilijumuika vitani katika nchi jirani ya Congo, huku ikiendesha vita vyake nyumbani dhidi ya jeshi la waasi Lord's Resistance Army.