KAMPALA. Mtangazaji afikishwa mahakamani
15 Agosti 2005Matangazo
Mtangazaji aliyeikasirisha serikali ya Uganda kwa matamshi makali juu ya kilichosababisha kifo cha aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan John Garang leo alifikishwa mahakami mjini Kampala na kukanusha kesi ya uchochezi dhidi yake.
John Mwenda mtangazaji wa kituo kimoja cha FM mjini Kampala aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki 5 za Uganda sawa na dola 247 za Kimarekani pesa taslimu na dhamana nyingine ya shilingi milioni kumi kutoka kwa wadhamini 5.
Mwenda alibaki korokoroni huku wenziwe wakijitayayarisha kukusanya fedha za dhamana kabla kuachiliwa kwake.
Mkurugenzi wa gazeti la Monitor na mmiliki wa kituo cha KFM bwana Conrad Nkutu amesema kuwa hatua hiyo ya serikali ya Uganda inahujumu uhuru wa vyombo vya habari.