KAMPALA: Milton Obote amefariki dunia
11 Oktoba 2005Matangazo
Rais wa zamani wa Uganda,Milton Obote amefariki dunia katika hospitali nchini Afrika ya Kusini,akiwa na umri wa miaka 81.Obote alikuwa rais mara mbili nchini Uganda na mara zote mbili aliondoshwa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.Hayati Obote alikuwa akiishi uhamishoni nchini Zambia.