Kampala. Mashirika ya kutoa misaada yafurajia makubaliano ya amani.
30 Agosti 2006Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kutoa misaada pamoja na umoja wa mataifa kaskazini mwa Uganda leo yamesifu makubaliano ya kihistoria ya kusitisha uhasama yenye lengo la kumaliza karibu miaka 20 ya vita vya kikatili, na wametoa wito wa kukamilishwa kwa haraka kwa makubaliano ya amani.
Siku moja baada ya makubaliano hayo kuanza kufanyakazi, makundi hayo yameitaka serikali ya Uganda na waasi wa Lord’s resistance Army kukubaliana kumaliza mzozo huo ambao unafahamika kila mara kuwa ni mmoja kati ya maafa makubwa ya kiutu duniani.
Vita kaskazini mwa Uganda vimeliingiza eneo hilo katika hali mbaya, na kusababisha mamia kwa maelfu ya watu kuuwawa, wengine wanaokadiriwa kufikia milioni mbili wamekimbia makaazi yao na kuwalazimisha wananchi kuishi katika hali mbaya , ambayo inahusishwa mara nyingi na waasi.