KAMPALA. maelfu waandamana kuunga mkono makubaliano ya kusimamisha vita
31 Agosti 2006Matangazo
Maelfu ya raia wa Uganda wamefanya maandamano huku wakipeperusha vitambaa vyeupe ishara kuwa wanaunga mkono makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliyotiwa saini jumamosi iliyopita kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa LRA wa kaskazini mwa Uganda wanao ongozwa na Joseph Kony.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kumaliza mojawapo ya vita vya muda mrefu katika bara la Afrika.