KAMPALA: Maandamano mjini Kampala kupinga rais asijiongezee muda.
25 Machi 2005Matangazo
Takriban watu 1,000 wanaounga mkono upinzani nchini Uganda wamefanya maandamano kupitia barabara za mji mkuu wa Kampala kupinga azma ya serikali ya rais Yoweri Museveni wa Uganda ya kutaka katiba ya nchi hiyo irekebishwe ili iweze kumpa fursa ya kugombea kipindi cha tatu cha urais.
Rais Museveni ameliongoza taifa la Uganda tangu mwaka 1986 na kipindi chake cha pili uongozini kinamalizika mwaka ujao.