KAMPALA: Kura ya maoni kuhusu katiba
29 Julai 2005Matangazo
Raia nchini Uganda wamepiga kura ya maoni kuamua kama mfumo wa kidemokrasia wa kuruhusu vyama vingi vya kisiasa urudishwe nchini humo,baada ya kupigwa marufuku kwa takriban miaka 20.Kura ya maoni ni hatua ya mwanzo ya kuibadilisha katiba ya Uganda,ambayo huzuia mfumo wa vyama vingi vya kisiasa.Makundi ya upinzani yamesusa kupiga kura yakisema,haki za kisiasa za msingi,hazihitaji kuidhinishwa na wapiga kura.