KAMPALA. Kituo cha FM chafungwa
12 Agosti 2005Matangazo
Serikali ya Uganda imesimamisha kwa muda usio julikana leseni ya utangazaji ya kituo kimoja cha Fm mjini Kampala baada ya mtangazaji maarufu kufanya kipindi kilichojadili juu ya kifo cha aliyekuwa makamu wa rais wa kwanza wa Sudan John Garang aliyefariki katika ajali ya helikopta ya rais wa Uganda Yoweri Museveni julai 30.
Mapema jana mjini Khartoum bwana Salva Kiir aliapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais mpya baada ya kufariki Garang.