KAMPALA: Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye afikishwa mahakamani
15 Novemba 2005Mtu mmoja ameuawa na polisi nchini Uganda katika siku ya pili ambapo watu wanapinga kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kiongozi wa upinzani nchini humo bwana Kizza Besigye.
Wakati polisi wakitumia mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya waandamanaji bwana Besigye alikuwa anasomewa mashtaka juu ya uhaini na ubakaji.
Watu wanaomwuunga mkono bwana Besigye wanaamini kwamba kukamatwa kwake ni sehemu ya njama za kumzuia kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka kesho.
Ikiwa atapatikana na hatia ya kosa la uhaini, kiongozi huyo wa upinzani na washtakiwa wengine 22, wanaweza kupewa adhabu ya kifo.
Mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yamelalamika juu ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa bwana Kizza Besigye.