Kamil Idris ateuliwa waziri mkuu mpya wa Sudan
20 Mei 2025Matangazo
Mkuu wa jeshi la Sudan na kiongozi wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan amemteua afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kamil Idris kuwa waziri mkuu mpya, zaidi ya miaka miwili ya vita vya umwagaji damu.
Idris, ambaye ni mwanadiplomasia msomi na mgombea urais wa zamani, aliwahi kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la haki miliki na pia amewahi kuhudumu katika ubalozi wa kudumu wa Sudan katika Umoja wa Mataifa.
Vita vya Sudan miaka miwili baadae, hali bado ni mbaya
Idris anachukua nafasi ya mwanadiplomasia mkongwe Dafallah al-Haj Ali ambaye aliteuliwa na Burhan mwishoni mwa mwezi Aprili na kuhudumu kwa kipindi cha chini ya wiki tatu kama kaimu waziri mkuu.