Uturuki yaendelea kuwakamata waandamanaji mjini Istanbul
29 Machi 2025Uturuki imezidisha ukandamizaji wake dhidi ya maandamano ya kuipinga serikali, ikimkamata wakili wa meya wa Istanbul aliyefungwa jela na kuwalenga waandishi wa habari zaidi. Nchi hiyo inakabiliwa na wimbi kubwa la machafuko katika zaidi ya muongo mmoja.
Siku tisa baada ya kukamatwa na kufungwa jela meya maarufu wa upinzani wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, waandamanaji walimiminika tena mitaani licha ya kuongezeka kwa hofu.
Wakili wa mwanasiasa huyo ambaye pia amekamatwa Mehmet Pehlivan, alisema kupitia chapisho la kwenye mtandao wa X kwamba Imamoglu anayeonekana kama mpinzani mkubwa wa kisiasa wa Rais Recep Tayyip Erdogan, ametiwa mbaroni kwa madai ya uongo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ameelezea wasiwasi juu ya namna Ankara ilivyoshughulikia maandamano.