MigogoroSyria
Kamanda wa SDF ayasifu makubaliano na serikali
11 Machi 2025Matangazo
Abdi ameandika kupitia mtandao wa X leo Jumanne kwamba watahakikisha wanajenga mustakabali bora kwa kuzingatia haki za Wasyria wote na kutimiza matarajio yao ya amani na utu.
Ofisi ya Rais nchini Syria ilitangaza jana Jumatatu juu ya makubaliano na SDF ya kuzijumuisha kwenye serikali ya kitaifa, taasisi za eneo inalolitawala la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Makubaliano hayo yamefikiwa katika wakati tete, ambapo Rais wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa akishughulikia mauaji ya watu wa jamii ya wachache ya Alawite, katika ghasia zinazotishia juhudi zake za kuiunganisha Syria baada ya mzozo wa miaka 14.