Kamanda wa NATO asema mifumo ya Patriot kupelekwa Ukraine
17 Julai 2025Matangazo
Kamanda mkuu wa kijeshi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Alexus Grynkewich amesema hivi leo kwamba maandalizi yanaendelea kuihamisha kwa haraka mifumo ya ziada ya ulinzi wa anga aina ya Patriot kuipeleka nchini Ukraine.
Kauli hiyo imetolewa wakati Ukraine ikiendelea kukabiliwa na baadhi ya mashambulizi mazito ya Urusi katika vita hadi sasa.
Grynkewich ameuambia mkutano katika mji wa Ujerumani wa Wiesbaden kwamba wanashirikiana kwa karibu na Wajerumani kuhusu usafirishaji wa mifumo hiyo ya Patriot haraka iwezekanavyo.
Wakati hayo yakiarifiwa Urusi imesema imezitungua droni 126 za Ukraine katika mashambulizi yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi raia wanne.