Kaja Kallas aitaka Marekani kumshinikiza Putin zaidi
31 Machi 2025Wakati wa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya mjini Madrid, Uhispania, Kallas amesema anafikiri Marekanipia ina jukumu katika kuweka shinikizo dhidi ya Urusi kumaliza vita hivyo.
Urusi inapaswa kusitisha vita na kuchukuwa hatua za mbele
Ameongeza kuwa lazima Urusi ikubali kusitisha vita vyake Ukraine na kuchukuwa hatua mbele. Hii inaweza kwa mfano, kujumuisha kuwarudisha watoto wa Ukraine au kuwaachilia wafungwa wa kivita.
Russia, USA, zakubaliana kufikisha mwisho vita Ukraine
Mbali na Kallas, mawaziri wa mambo ya nje kutoka Poland, Ufaransa na Uhispania, pamoja na kamishna wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya Andrius Kubilius, pia walishiriki katika mazungumzo hayo ya vita vya Urusi vinavyoendelea nchini Ukraine.
Tamko la pamoja linatarajiwa mwishoni mwa mkutano huo, ambao pia unatarajiwa kuangazia juhudi za sasa za Trump za usitishaji mapigano.