Kadhi Mkuu wa Kenya Abdulhalim Hussein afariki dunia
10 Julai 2025Kulingana na familia yake, hali yake ilionesha dalili za kuimarika baada ya safari hiyo ya matibabu.
Kifo chake kilitangazwa rasmi na Sheikh Jamaludin Osman ambaye ni imamu mkuu katika msikiti wa Jamia mjini Nairobi.
Kadhi Abdulhalim aliteuliwa Julai 2023 kushika nafasi hiyo baada ya kupitia mchakato wa uteuzi uliofanywa na Kamisheni ya huduma za mahakama.
Alikuwa miongoni mwa wagombea watano walioteuliwa kuchukua nafasi ya Kadhi Mkuu aliyekuwepo wakati huo Sheikh Ahmed Muhdhar, aliyekuwa anastaafu baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 12.
Miongoni mwa majukumu ya marehemu Sheikh Abdulhalim yalikuwa ni pamoja na kusimamia kesi za kifamilia za waumini wa Kiislamu, zinazohusisha mirathi, talaka na ndoa.
Marehemu ataswaliwa baada ya swala ya Alasiri katika msikiti wa Masjid Noor, Bondeni katikati mwa mji wa Mombasa na atazikwa kwenye makaburi ya Kikowani.