KABUL:Waziri wa nje wa Marekani ziarani Afghanistan
13 Oktoba 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice ameizuru Afghanistan wakati machafuko mapya yakitokea na wanamgambo wa Kitaliban wakilaumiwa kuhusika na mashambulio hayo.Makombora yaliripuka katika mji mkuu Kabul na kuwauwa wanajeshi 6 na wafanyakazi 5 wa mashirika ya misaada. Katika jimbo la kusini la Kandahar,washambuliaji wa Kitaliban waliwauwa pia madaktari 2, wanesi 2 na dreva wa shirika moja la misaada la Afghanistan.Bibi Rice baada ya kukutana na rais Hamid Karzai wa Afghanistan alisisitiza kuwa Marekani itaendelea kuisaidia nchi hiyo katika miaka ijayo.