Kabul.watu 16 wauwa kwa bomu la kujitoa muhanga Afghanistan.
8 Septemba 2006Bomu linalokisiwa kuwa ni la kujitolea muhanga katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul limeuwa kiasi cha watu kumi na sita wakiwemo wageni saba.
Mripuko huo wa bomu ulitokea katika moja ya mitaa yenye shughuli nyingi za kijamii na unaolindwa kwa hali ya juu ikiwa ni nn’je tu ya ubalozi wa Marekani.
Vyombo vya habari vya kiarabu vimeripoti kuuwawa kiasi cha wanajeshi watatu wa kimarekani.
Wapiganaji wa kitaliban walianza kushambulia kwa mabomu ya kujitolea muhanga wishoni mwa mwaka jana ikiwa ni moja kati ya mikakati yao ya kudhoofisha vikosi vya kijeshi vya magharibi nchini Afghanistan na pia kuiyumbisha serikali ya rais Hamid Karzai.
Shambulio hili la leo limetokea wakati wakuu wa NATO wanakwenda kukutana Poland kwa nia ya kutaka kuidhinishwa wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini Afghanistan, ambako jenerali wa kiingereza alitahadharisha kuwa, mashambulio ya kujitolea muhanga nchini humo ni ya hatari zaidi kuliko nchini Iraq.