Kabul.Wanajeshi wa Uingereza wajeruhiwa kwa bomu la kujitolea muhanga.
4 Septemba 2006Matangazo
Bomu lililotegwa kwenye gari limeripuka karibu na wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakipiga doria katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
Shambulio hilo limewauwa wa-Afghanistan wanne na kuwajeruhi wanajeshi wanne wa Kiingereza.
Polisi wa Afghanistan wamesema, hilo lilikuwa shambulio la kujitolea muhanga na kuongeza kuwa, mwanajeshi wa kugeni pia aliuwawa, lakini ISAF majeshi ya kimataifa yanayolinda usalama chini ya uongozi wa NATO hayakuweza kuthibitisha ripoti yoyote ile.
Mara kwa mara miripuko ya aina hiyo huwa inatokea kwenye bara bara kuu inayoelekea n’je ya mji mkuu kupitia kando ya viwanja vya ISAF na Umoja wa Mataifa na pia vituo vya majeshi ya Afghanistan.