KABUL:Mwanajeshi wa kulinda amani ameuawa Afghanistan
14 Novemba 2005Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan mjini Kabul,askari jeshi mmoja wa Kijerumani wa vikosi vya kimataifa vinavyolinda amani nchini Afghanistan-ISAF ameuawa katika shambulio la bomu.Mashahidi wamesema bomu la pili lililotegwa kwenye gari liliripuka karibu na eneo la shambulio la kwanza dakika 90 baadae.Maafisa wa polisi mjini Kabul wamesema shambulio la kwanza liliwajeruhi pia wanajeshi wengine 2 wa Kijerumani na si chini ya raia 3.Wakuu wa majeshi ya Ujerumani mjini Potsdam wamearifu kuwa gari la ISAF lililokuwa na wanajeshi wa Kijerumani lilishambuliwa lakini hawakueleza zaidi.