KABUL:Mwanajeshi wa Kingereza ameuawa Afghanistan
27 Agosti 2006Matangazo
Mwanajeshi wa Kingereza kwenye kikosi kinachoongozwa na NATO nchini Afghanistan,ameuawa katika mapigano yaliyozuka dhidi ya waasi wa Taliban katika wilaya ya Helmand kusini mwa nchi.Wizara ya ulinzi ya Uingereza,imethibitisha kifo cha mwanajeshi huyo.Siku ya Jumamosi, wanajeshi 2 wa Ufaransa waliuawa katika shambulio la bomu kwenye wilaya ya Laghman,mashariki mwa Afghanistan.