KABUL.Mlipuko watokea katika kambi ya ujenzi ya Ujerumani
29 Agosti 2005Matangazo
Kumetokea mlipuko katika kambi ya ujenzi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck alipanga kuzuru maeneo ya Faisabad na Kundus nchini Afghnistan.
Msemaji wa jeshi amesema, kwamba hakuna mtu yeyote aliye jeruhiwa ijapokuwa uharibifu wa kiasi umetokea na uchunguzi unafanywa kutafuta chanzo cha mlipuko huo.
Kwengineko huko Ufilipino bomu lilofichwa ndani ya ferry kusini mwa Ufilipino lili lipuka na kuwajeruhi takriban watu 30 wakiwemo pamoja watoto 9.
Msemaji wa jeshi katika kisiwa cha Basilan amesema hadi kufikia sasa hakuna mtu aliyetangaza kuhusika na shambulio hilo, hata ingawa kundi la waislamu wenye itikadi kali la Abu Sayyaf linashukiwa huenda limehusika na shambulio hilo la bomu.